Je ni kweli Muziki na Soka ndio mkombozi aliyebaki kwa Vijana? baadhi ya Wadau wameamua kufunguka!!
wanamuziki wanaokua kimuziki au kujaribu kupanda kutoka chini a.k.a underground(s)
wapata fursa ya kuwakuza kimuziki,na pia kuweza kuwakwamua kutoka katika janga la Umaskini,
asema hayo mmiliki wa moja ya studio kubwa nchini(jina kapuni) baada ya kupokea habari na
pia kushuhudia kujaa kwa studio mpya ambazo kwasasa zipo karibu kila kona ndani ya jiji hili
la dar es salaam.na zimekuwa zikileta upinzani mkali sana! na aliendelea kukandamiza kwamba,
inavyosemekana baadhi ya studio hizi zina ubora wa kimataifa ingawa nyingi zake bado(feki) ni
kwa madhuni ya demo(yani baada ya kurekodi ni kwaajili ya kumpelekea producer mkumbwa na sio redioni)
.akaendelea, hivyo kutokana na fursa hiyo ma producers nao wamepata changamoto ya kupandisha ubora
ili kuweza kuwarahisishia wale wenye vipaji kweli wawe na mafanikio makubwa kimuziki. Bila kusita
jarida hili likafanya uchunguzi zaidi kwa kutembelea kwenye baadhi ya studio yani zilizopo kati ya
zile kubwa(zenye majina) na zile ndogo(ambazo azijulikani kabisa),na kugundua ongezeko la idadi ya
wasanii chipukizi a.k.a underground(s) na bei pia kutoka 200000/=tsh mpaka 250000/=tsh kwa track moja.
na kwa upande wa soka, mdau wa soka Musa A. Mfawidhi amesema kwamba, vijana mbalimbali wameanza kujikita
mazoezini kwaajili ya kuchaguliwa na viongozi wa academy za soka nchini na nje ya nchi ili waendelezwe
kufikia level za usajili wa donge nono nchini au nje ya nchi..
Mh:John Paul
Mfatiliaji wa maswala ya Vijana na Mwandishi kutoka (Wise Men Council)
wisdomtimez.blogspot.com
Comments
Post a Comment