kutana na sababu zinazofanya wasanii walioendelea nchini kuwa binafsi na kuleta mapinduzi yasiyofaa/uaribifu!!
Ongezeko la kipato pamoja na kujiona tayari wapo kwenye system vimefanya wasanii wamesahau kuwa wao wananguvu kubwa
katika jamii kwenye upande wa kuleta mabadiliko kiakili au kimaendeleo ya kiuchumi kwa wakati. wanashindwa kugundua
au wanafanya makusudi au ni ukosefu wa maarifa ambao unafanya wasanii kusahau kwamba wao ni kioo cha jamii, mambo
wanayofanya sasa ni kutokana na kuiga kutoka nchi za wenzetu, lakini wanashindwa kuelewa kwamba watu wanaowaiga ni
watu waliofikiria hayo mambo kutoka kwenye akili zao kulingana na nchi zao! sasa inakuwaje sisi na nchi yetu hii yenye
majanga ya kutosha tunashindwa kuleta itikadi za maendeleo? angalia baadhi ya wacheza mpira wa Africa magharibi wanaocheza
ulaya (ni watu wa itikadi za kusaidia jamii zao) kuleta mapinduzi ya kimaendeleo, ingawa nao wanastarehe zao lakini hawajabweteka
kama wasanii wetu.
je harakati zipi analeta msanii unayemkubali?
angalia isije ikawa unamkubali mpumbavu!!
kama wewe ni mwanaharakati unaweza ku share huu ujumbe kwa kubonyeza vitufe vya mitandao hapo chini.
Comments
Post a Comment