Serikali imekubaliana na Benki ya CRDB, PROGRAMU YA KUKUZA AJIRA KWA VIJANA WAHITIMU WA VYUO VYA ELIMU YA JUU.

Kwa kuwa kasi ya wanaojiunga elimu ya juu nchini imeongezeka wastani wa (48% kwa mwaka) na Wizara imeona vijana wanapomaliza elimu ya juu wanakuwa na elimu ya nadharia katika fani walizozisomea ,tumeona kuna umuhimu wa elimu ya ujasiriamli, mitaji na maeneo ya kufanyia uzalishaji na biashara ambavyo ni msingi wa programu hii. Programu hii ni bora kwa kuwa ina vigezo vya ufuatiliaji na tathimini ya utekelezaji.

LENGO:
Lengo kuu la program ni kuongeza fursa za Ajira 30,000 za moja kwa moja kwa vijana wahitimu wa elimu ya juu kwa kipindi cha miaka mitatu (3) na kuwawezesha vijana kujiajiri na hata kuajiri vijana wengine kutokana na miradi watakayoibuni wao wenyewe.

MIRADI.
Miradi itakayoanzishwa itatoa ‘Mnyororo mzima wa thamani’ au INTERGRATED CROSS
VALUE CHAIN (ICVC)
Kwa mfano,mradi wa Alizeti na ukamuaji mafuta.
1st step- Uandaaji mashamba,ulimaji,upandaji,palizi na uvunaji
2nd step- Usafirishaji, uhifadhi, usindikaji
3rd step- Ukamuaji mafuta, ufungashaji na uuzaji mafuta.

PROGRAMU ITAJUMUISHA YAFUATAYO.
I. Utambuzi na uhamasishaji vijana—ambapowataandikishwa kupitia mikoa na Wilaya wanayoishi
II. Kutoa mafunzo ya ujasiria mali na stadi zakazi-mafunzo yatatolewana SUA,baadae kwani kubuni na kuandaa andiko la Biashara (Business proposal)
III. Kujenga uwezo wa vijana kulingana na miradi waliyoainisha –lengo ni kuwapatia ujuzi na uzoefuwa namna ya utekelezaji miradi.
IV. Mafunzo na uzoefu kwa waendeshaji wa program-Wahusika watajengewa uwezo kujifunza kutokana na miradi ya ukuzaji ajira katika nchi nyingine.Taasisi husika Wizara ya Kazi na Ajira,Benki ya CRDB,SUA na SUGECO.
V. Kutoa mafunzona huduma za kitaalamu na uratibu katika maeneo ya uzalishaji.

UTARATIBU WA UKOPESHAJI.
 Program hii ni ya miaka 3 na mikopo itakayotolewa ni ya miaka 3 na urejeshwaji wa mikopo ni kuanzia miaka3 hadi 5.
 Muda wa mkopaji kurejesha mkopo ni kuanzia miezi 6 hadi mwaka 1 kutegemeana na aina ya mradi.
 Utaratibu wa ukopeshaji ni wastani wa sh.Mil 50 hadi 300mil kulingana na mradi.
Utaratibu wa utekelezaji na viwango vya riba utaainishwa katika mpango kazi wa utekelezaji programu.

NAPIA KUNA FULSA NYINGINE..


IPTL kusaidia miradi ya kuwawezesha vijana kiuchumi

Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni ya ufuaji umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), Bw. Harbinder Signh Sethi (kushoto) na Katibu na Mwanasheria Mkuu wa kampuni hiyo Bw. Joseph Makandege (wapili kushoto) wakikabidhi hundi ya shilingi milioni 11 kwa mwakilishi wa Kanisa la Mt. Rita Wakashia lililopo Kimara jijini Dar es Salaam, George Kashushura. Fedha hizo zitatumika kuanzisha SACCOS ya kanisa hilo, lenye lengo la kuwainua vijana kiuchumi. Makabidhiano hayo yalifanyika jijini Dar es Salaam jana ======  =======  ======= IPTL kusaidia miradi ya kuwawezesha vijana kiuchumi  
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya ufuaji umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) imeanza utekelezaji wa mpango wake wa kuiwezesha miradi mbali mbali inayowawezesha vijana wakitanzania kuimarika kiuchumi, ikiwa na lengo la kukuza maendeleo ya uchumi nchini.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi hundi ya shilingi milioni 11 kwa kikundi cha kwaya cha kanisa la Mtakatifu Rita Wakashia lililopo Kimara jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti Mtendaji wa IPTL, Bw. Harbinder Singh Sethi alisema kampuni yake imejidhatiti katika kuhakikisa inatekeleza mipango yake ya kupiga jeki miradi ambayo itasaidia kuondoa umasikini na ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana nchini Tanzania.
“Hizi milioni 11 tulizotoa kwa Kanisa la Mt. Rita Wakashia, ambazo zitatumika katika uanzishwaji wa SACCOS kwa wanakwaya wa kanisa, ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wetu wa kuchangia katika kusaidia miradi ya kijamii na ya kiuchumi unaolenga kusaidia vijana wa kitanzania kuwa wachangiaji wakubwa katika ukuaji wa uchumi nchini,” alisema Singh.
Bw. Harbinder alisema mpango huo pia unalenga kusaidia mashule, makanisa, misikiti na makampuni mengine yasiyotengeneza faida yanayofanyakazi ili kuwawezesha vijana kuwa mstari wa mbele katika kuchangia maendeleo ya kiuchumi Tanzania.
“Tunaamini kuwa SACCOS hii itakayoanzishwa itatoa fursa nzuri ya kujiwekea akiba nakutumika kama  chanzo cha mikopo kwa vijana na wanakwaya wengine wa kanisa. Hii ni hatua kubwa katika kujikwamua kiuchumi katika jumuiya hii ya kanisa, ambayo ni taasisi isiyotengeneza faida,” alisema.
Naye Katibu na Mwanasheria Mkuu wa IPTL, Bw. Joseph Makandege alisema ili kuwapa sauti vijana na kuwaongezea fursa za kujiimarisha kiuchumi, IPTL kwa kushirikiana na kampuni ya Pan African Power (PAP) imetenga sehemu ya pato lake kwa ajili ya kupiga jeki miradi ya maendeleo ya kijamii, kwa dhamira ya kusaidia miradi ya kimaendeleo inayowalenga vijana.  
“Sisi kama IPTL na PAP, tumeona kuwa ni jukumu letu kuisaidia jamii inayotuzunguka. Kwa kuanzisha SACCOS, ninaimani vijana wa kanisa la Mt. Rita Wakashia wataweza kuanzisha mradi madhubuti utakaowaletea mabadiliko chanya ya kiuchumi. Hii ndiyo sababu tulishawishika kutoa mtaji huu wa kuanzia ili kuwawezesha kuanzisha SACCOS,” alisema Bw. Makandege.   
Akizungumza kwa niaba ya wanakwaya na waumini wengine wa kanisa hilo, Bw. George Kashushura alizishukuru IPTL na PAP kwa msaada wao na kubainisha kuwa fedha iliyotolewa itaelekezwa katika malengo mazuri yatakayobadilisha maisha ya vijana walio wengi.
“Fedha tulizopokea leo hii zitatumika kama mtaji wa kuanzisha SACCOS yetu ya kanisa ambayo itakuwa ni chachu ya mabadiliko ya maisha ya vijana walio wengi katika kanisa letu,” alisema Kashushura.

Comments

Popular posts from this blog

Wise Men Council - The Vision

Here is Another way you can Support us to reach our goal(New and Used Items)for Sale.