Imeonekana itasaidia kama selikali itafungua au kuanzisha kampeni za kusaidia au kuchangia kwenye mipango waliyonayo vijana kwenye secta ya maendeleo yao kiuchumi.

inavyosemekana kama vijana watapata fursa ya kusikilizwa na secta maalumu za Selikali ili kuwaendeleza kiuchumi na kuyaweka
mawazo yao katika vitendo, kwa kuyafanyia kampeni kubwa kama zile za malaria na ukimwi. Idadi kubwa ya vitongoji, wilaya
na hata mikoa kutabadilika na kuleta manufaa yenye nguvu ya kutukomboa katika janga hili la umaskini. Vijana wamekuwa
wakiahidiwa vitu vingi bili kufikia  matekelezo! kuna mipango mbalimbali ambayo vijana tunatakiwa kushiriki kitaifa na hata kimataifa,
sema kutokana na upungufu kama sio uhaba wa mawasiliano,vijana wa nchi hii bado tupo nyuma katika fursa hizo..tumegundua badala
ya kulaumu! sasa tunatakiwa kupiga mbiu ili selikali ituwekee mkazo kwa kusudi!! ili maisha mbeleni yasituwekee vikwazo ambavyo vilikuwa ndani ya uwezo
wetu! jarida hili limefanya uchunguzi na kubaini kwamba idadi kubwa ya vijana inapotea kwa kukosa ushirikiano mzuri na selikali
yao. je ukiwa kama kijana tuendelee kukaa kimya na kusubiri? au tuamke na kuimarisha juhudi zetu?

NOTE: Pamoja tunaweza kuwa Imara/Together we can be strong




Mh:John Paul
Mfatiliaji wa maswala ya Vijana na Mwandishi kutoka (Wise Men Council)

wisdomtimez.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

Wise Men Council - The Vision