Tamaa ya pesa na mafanikio ya fasta fasta vyatikisa nyavu nchi za nje!

kwa lengo la HARAKATI na sio upaparazi, habari hii imewasilishwa na mmoja wa wachunguzi wa maswala ya vijana
wa Jarida hili anayeishi Marekani.


Vijana wa nchi za EastAfrica, wamejikuta wakilazimika kucheza sinema za x nchi za nje, jarida hili limefatilia na kugundua
vijana wengi kutoka East Africa waishio ulaya na marekani wanaendelea kujipatia kipato cha hali ya juu kwa kucheza sinema
za uchi, inavyosemekana ni kwamba hakuna anayewalazimisha kuingia katika secta hizo, isipokuwa ni donge nono la wadau
wakubwa kutoka upande wa nchi hizo tajiri..Tumekuwa na mfatiliaji kutoka Tanzania aishie marekani(jina kapuni) amekandamiza
zaidi kwa kusema kwamba Tamaa ya pesa na mafanikio ya fasta fasta ndio chanzo cha vijana wetu kupagawa. mfatiliaji huyo
amekuwa akishuhudia matukio mbalimbali na kuamua kurusha habari kwa lengo la kuendelea kuamsha kampeni za vijana
dhidi ya umaskini..na kulingana na takwimu za Umoja wa vijana Africa kwa miaka mingi imeonekana vijana wa kuanzia miaka 15 hadi 35
kwa ufuatiliaji wa miaka 30   wengi wa vijana hawafikishi miaka 50 na hii ni kutokana na majanga waliojihusisha au kushiriki, likiwemo la
madawa ya kulevya, ujambazi, ngono zembe na utumiaji wa silaha kinyume cha sheria..
ukiwa kama kijana simama imara tuendeleze kampeni zidi ya umaskini..



Mh:John Paul
Mfatiliaji wa maswala ya Vijana na Mwandishi kutoka (Wise Men Council)

wisdomtimez.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

Wise Men Council - The Vision