Vijana wapotea,maisha yawa magumu waishia kwenye madawa ya kulevya na bangi huku wakidhani muziki na soka ndio wakombozi waliobakia..




kutokana na hali ya maisha kuzidi kuwa ngumu baadhi ya vijana wamezidi
kujikita katika matumizi na pia kushiriki kwenye biashara ya madawa ya
kulevya na mihadarati huku wakidai muziki ndo kitu cha uhakika na ukifatiwa
na soka.vijana wameonekana wakifadhaishwa na mipango ya kiselikali ya
kuwasaidia kiuchumi ili kuwakwamua katika janga zito la umaskini, jarida
hili limeongea na baadhi ya vijana na wameonekana wakipinga vikali msemo wa
"maendeleo ya vijana" kutoka selikalini.wengi wao wamedai bila muziki au
biashara ya madawa,kutoka kwao itakuwa ni ngumu sana,kwani soka nalo bado halijajikita
sawasawa kufanya wawe na maendeleo kiuchumi. huku wasomi nao wakidai kazi zimekuwa
ngumu kupata na kwa hali ilivyo sasa kujiendeleza ki elimu kwao ni upotevu wa fedha
na ni bora wajikite kwenye biashara.
tumejaribu kumtafuta muhusika msemaji wa selikali kuhusu"maendeleo ya vijana" ili
atupe ushirikiano kwenye jambo hili,kwa bahati mbaya jitihada ziligonga mwamba..

Mh:John Paul
Mfatiliaji wa maswala ya vijana na Mwandishi kutoka (Wise men Council)

wisdomtimez.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

Wise Men Council - The Vision