Viongozi washindwa kutambua kwamba watakapoondoka madarakani Vijana tutaingia!


kutokana na kushindwa kutuandalia mazingira mazuri na kutuwekea mikakati ya maendeleo
vijana wameamua kuweka wazi kwamba utafika wakati wa kuchukua madaraka na hapo
ndipo patakapoleta shida kutokana na misingi ambayo wakuu wetu walishindwa kutujengea!
kwasasa inaonekana kama jambo la kawaida ila ni mtihani unaohitaji majibu ya haraka sana,
kulingana na utafiti uliofanywa na jarida hili, imeonekana wanaofaidika ni wachache na pia ni wale
ambao wapo kwenye mstari! au kwa lugha nyingine ni wale walio na uhusiano na wakuu.
mpaka sasa  ni kila mmoja akijipigania..na kwajinsi hali ilivyotata inaonekana hakuna atayekuja
kuwa tayari kusimamia au kusaidia waliopo kwenye nyazfa(watakapofikia ustaafu/uzee) kwa kile
 wanachokifanya sasa!!

zimeitishwa kampeni mbalimbali ambazo zingeleta usaidizi kwa vijana lakini mkazo umekuwa ni mdogo
sana na hata tukifatilia tumekuwa tukipigwa kalenda,na pia ni sawa na "kumpigia mbuzi gitaa" mmoja wa
 wasemaji wa kikundi cha maendeleo ya vijana ambaye hakupenda jina lake litajwe kwasababu za KIUSALAMA
amesema ni ngumu sana kwasababu pande zote mbili hazijafikia kuwa na nia moja kutokana na sababu za
maendeleo ya kibinafsi..

je ukiwa kama kijana unaimarikaje kwenye jamii yako?


Mh:John Paul
Mfatiliaji wa maswala ya vijana na Mwakilishi kutoka (Wise men Council)

wisdomtimez.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

Wise Men Council - The Vision