Serikali imekubaliana na Benki ya CRDB, PROGRAMU YA KUKUZA AJIRA KWA VIJANA WAHITIMU WA VYUO VYA ELIMU YA JUU.
Kwa kuwa kasi ya wanaojiunga elimu ya juu nchini imeongezeka wastani wa (48% kwa mwaka) na Wizara imeona vijana wanapomaliza elimu ya juu wanakuwa na elimu ya nadharia katika fani walizozisomea ,tumeona kuna umuhimu wa elimu ya ujasiriamli, mitaji na maeneo ya kufanyia uzalishaji na biashara ambavyo ni msingi wa programu hii. Programu hii ni bora kwa kuwa ina vigezo vya ufuatiliaji na tathimini ya utekelezaji. LENGO: Lengo kuu la program ni kuongeza fursa za Ajira 30,000 za moja kwa moja kwa vijana wahitimu wa elimu ya juu kwa kipindi cha miaka mitatu (3) na kuwawezesha vijana kujiajiri na hata kuajiri vijana wengine kutokana na miradi watakayoibuni wao wenyewe. MIRADI. Miradi itakayoanzishwa itatoa ‘Mnyororo mzima wa thamani’ au INTERGRATED CROSS VALUE CHAIN (ICVC) Kwa mfano,mradi wa Alizeti na ukamuaji mafuta. 1st step- Uandaaji mashamba,ulimaji,upandaji,palizi na uvunaji 2nd step- Usafirishaji, uhifadhi, usindikaji 3rd step- Ukamuaji mafuta, ufungashaji na uuzaji mafuta. PROGR...